Swahili Kanuni za Maadili kwa Mgavi wa World Vision

Download
inclusion
Monday, October 23, 2023

World Vision International (WVI) imejitolea kwa dhati kuzingatia viwango vya juu zaidi vya maadili katika shughuli zake zote za manunuzi. Kanuni hii ya maadili inatoa taratibu na tabia katika mwenendo wa kila siku wa utendaji kuhakikisha manunuzi yanayotambulika kimataifa, maadili na kanuni za biashara bora zinafuatwa. Ili kuhakikisha World Vision/Vision Fund (VF)na wadau husika wanakidhi matakwa ya wafadhili, tutazingatia kanuni za mahitaji ya ununuzi ya wafadhili pale inapohitajika/inapobidi. Kwa hiyo, WV/VF inatarajia wasambazaji wake, wakandarasi wakubwa na wadogo kusaini Kanuni za Maadili na kukiri kukubaliana na kufuata kanuni zilizopo kama ifuatavyo