Kanuni za Maadili kwa Mgavi wa

 

Kanuni za Maadili kwa Mgavi wa World Vision

World Vision International (WVI) imejitolea kwa dhati kuzingatia viwango vya juu zaidi vya maadili

katika shughuli zake zote za manunuzi. Kanuni hii ya maadili inatoa taratibu na tabia katika

mwenendo wa kila siku wa utendaji kuhakikisha manunuzi yanayotambulika kimataifa, maadili na kanuni za biashara bora zinafuatwa. Ili kuhakikisha World Vision/Vision Fund (VF)na wadau husika

wanakidhi matakwa ya wafadhili, tutazingatia kanuni za mahitaji ya ununuzi ya wafadhili pale inapohitajika/inapobidi. Kwa hiyo, WV/VF inatarajia wasambazaji wake, wakandarasi wakubwa na wadogo kusaini Kanuni za Maadili na kukiri kukubaliana na kufuata kanuni zilizopo kama ifuatavyo.

 

WV/VF inatarajia wasambazaji wake:

 

1) Kujitahidi kuboresha thamani ya pesa -

             a) Kutafuta kikamilifu kuonesha na kuboresha matokeo, na kupunguza gharama za maisha kupitia         makubaliano, na/au oda ya manunuzi.

             b) Kuweka bei elekezi  kwa uaminifu kuakisi  uhalisia na vihatarishi vinavyoweza kujitokeza.

 

2) Tenda kwa weledi na uadilifu -

            a) Kuwa mwaminifu na mkweli wakati wa zabuni.

            b) World Vision inatarajia kwamba wasambazaji wake wanahimiza na kufanya kazi na wasambazaji wao wenyewe na wakandarasi wadogo ili kuhakikisha kwamba wanafuata kanuni za Maadili, na kuwa na uwezo wa kufanya kwa vitendo inapohitajika.

            c) Kutenda kwa namna ambayo inachochea maendeleo na mahusiano chanya na yenye maadili ya biashara na WV/VF.

           d) Kuonyesha dhamira ya wazi na thabiti kwa ushirikiano na uwajibikaji wa kijamii.

 

3) Kuwajibika –

         a) Tumia miundo ya bei ambayo inalinganisha malipo kwa matokeo yanayoakisi zaidi kugawana hasara za kiutendaji.

        b) Kutarajia kuwajibika kwa matokeo yasiyotarajiwa na kukubali kuwajibika kwa matokeo hayo ikiwa ni pamoja na kuwa mwaminifu pale mambo yanapoharibika ili kujifunza.

 

4) Kuwa pamoja na WV/VF -

         a) Kuwa tayari kufanya kazi katika ofisi zote za WV/VF, ikijumuisha katika maeneo hatarishi na yaliyoathiriwa na migogoro.

         b) Kushirikisha na kuhawilisha ubunifu na ujuzi wa mbinu bora ili kuongeza ufanisi

 

5) Kubaliana kuepusha aina yoyote ya mgongano wa maslahi—

Mgavi au mkandarasi anathibitisha kwamba hana uhusiano, hana ubia wa kibiashara, kuhusika, nafasi, maslahi ya kifedha, na hajapokea zawadi yoyote, mkopo, au kujihusisha na muamala wowote unaohitaji ufichuzi chini ya  sera ya migongano ya maslahi na WV/VFT .

 

6) Kuzingatia mikataba ya kimataifa ya kazi na sheria inayotumika ya kazi/ajira.

 

7) Kuwa na sera thabiti ya mazingira –

       a) WV/VF inatarajia wasambazaji wake kuwa na sera madhubuti ya mazingira na kuzingatia sheria na kanuni zilizopo za kulinda mazingira.

 

Taarifa ya Shukrani ya Kanuni ya Maadili ya Wasambazaji wa WV

Saini yangu hapa chini inathibitisha kwamba mimi/sisi/mgavi, nimesoma na kuelewa kikamilifu na kukubaliana na  Kanuni za Maadili ya Mgavi wa World Vision zilizowekwa hapo juu kama zinavyotumika. Ninaelewa kuwa hatua yoyote kinyume na Kanuni hii ya Maadili ya Wasambazaji inaweza kusababisha kusitishwa kwa uhusiano wa kibiashara kati yangu na WV.

 

 

 

…………………………………………………………….                                     ……………………………………………..

Jina na cheo cha mwakilishi wa Msambazaji                                               Sahihi

 

…………………………………………………..                                               ……………………………………………………

Jina la kampuni/Msambazaji                                                                   Tarehe