Jenga familia inayozingatia lishe na afya bora

Mradi wa Uboreshaji Huduma za Lishe katika Kuimarisha Afya ya Uzazi kwa Mama na Mtoto (ENRICH)una lengo kuu la kuchangia kupunguza maradhi na vifo vya uzazi kwa mama na mtoto vinavyosababishwa na sababu za kilishe katika mikoa ya Shinyanga na Singida. Hii ni kwa njia ya utekelezaji wa hatua za gharama nafuu za lishe bora ambazo ni pamoja na: kuimarisha mfumo wa afya,kuendeleza mazao yaliyorutubishwa kibaiolojia, kuhamasisha ushiriki wa wanaume, na kushughulikia moja kwa moja utapiamlo ndani ya siku 1000 za kwanza za maisha ya mtoto.

Ingawaje ni mwaka mmoja sasa tangu kuanza kwa mradi, tumeshuhudia mabadiliko na maendeleo makubwa kuelekea matarajio yetu juu ya wanawake na watoto. Kupitia kufanya kazi na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, jamii, serikali za mitaa, timu za usimamizi wa afya ngazi za mkoa na wilaya pamoja na watoa huduma za afya, Mradi wa ENRICH umenufaisha vijiji 50 na vituo vya afya 58. Hili nina mchango madhubuti katika ubora wa upatikanaji wa huduma za lishe kwa watoto, wanawake wajawazito, wanawake wanaonyonyesha na jamii kwa ujumla.

Furahia usomaji wa ripoti hii